Mama Kanumba atoa la moyoni baada ya Lulu kuachwa 'huru'


Siku mbili tangu alipoachiwa muigizaji Elizabeth Michael ’Lulu’, mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema ameumia na tangu alipopata taarifa hizo hajalala

Akizungumza mama Kanumba amesema, tangu alipopata tetesi za msanii huyo ametoka jela, amejikuta anakosa usingizi na kuumwa presha

Ameongeza na kusema, kutokana na suala hilo, imemlazimu leo Jumatatu kwenda kwenye maombi kwa ajili ya afya yake hiyo

Amesema, licha ya kuwa si yeye aliyemuhukumu, Lulu alipaswa kukaa hata mwaka mmoja ili roho yake iridhike lakini ndio hivyo: "Siku zote maskini hana haki."

Hata hivyo,  amewashukuru wote waliohusika kumtoa na kuongeza kuwa yote ni kwa sababu yeye hana pesa na anajua watu wataanza kumtusi mitandaoni kwa sababu hiyo lakini yote anamuachia Mungu.

 Jeshi la Magereza kupitia Ofisa Habari wake, Lucas Mboje, limesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Mama Kanumba atoa la moyoni baada ya Lulu kuachwa 'huru' Mama Kanumba atoa la moyoni baada ya Lulu kuachwa 'huru' Reviewed by KUSAGANEWS on May 14, 2018 Rating: 5

No comments: