Watatu washambuliwa na mbogo


Watu watano, wakazi wa Kata ya Kirongo, wilayani Rombo, Kilimanjaro wamelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mbogo anayesadikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Karume iliyopo tarafa ya Usseri wilayani humo

Akizungumza Diwani wa kata ya Kirongo, Samanga Kimario amesema kuwa watu hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakitoka kanisani jana Jumapili

“Inasemekana walikuwa wanatoka kanisani na wakavamiwa na mnyama huyo na akawajeruhi sehemu mbalimbali za miili yao,” amesema

Kimario amesema kuwa mnyama huyo amezua taharuki kubwa na ya kihistoria kwani  haijawahi kutokea mbogo akaingia eneo hilo

Pia amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi aliwasiliana na maofisa wanyamapori ili kupata msaada zaidi wa kunusuru maisha ya wananchi

"Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusiana na mnyama huyo niliwasiliana na maofisa wanyamapori ili watusaidie na baadaye walifanikiwa kumuua mnyama huyo, " amesema Diwani Kimario.

Watatu washambuliwa na mbogo Watatu washambuliwa na mbogo Reviewed by KUSAGANEWS on May 14, 2018 Rating: 5

No comments: