Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Abdul Nondo ameiandikia barua Mahakama ya Wilaya ya Iringa kumkataa
hakimu John Mpitanjia anayesikiliza shauri lake
Nondo ambaye pia ni mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi
nchini (TSN), alisema anamtilia mashaka hakimu huyo hivyo ameona aiandikie
barua mahakama ili itende haki
Wakili wa Nondo, Jebra Kambole ndiye aliyewasilisha barua hiyo
ambayo imeeleza kuwa kuna mazingira yasiyo rafiki katika kesi hiyo. Baada ya
kuwasilisha malalamiko hayo, wakili wa Serikali, Abeid Mwanadalamo alidai
kujiondoa kwa hakimu kutakubaliwa iwapo tu malalamiko yaliyoletwa ni ya msingi
na ushahidi upo wazi
“Kama aliona kuna kasoro alitakiwa alete malalamiko yake
mwanzoni si leo,” alieleza
Mwandalamo alieleza kuwa hizo ni njama za kutaka
kuchelewesha shauri hilo na akaiomba mahakama kulitupilia mbali ombi hilo
Kambole alidai ni haki ya mshtakiwa kumkataa hakimu kama
anaona haki haitendeki
Baada ya maelezo hayo, hakimu Mpitanjia aliahirisha kesi
hiyo hadi Mei 16 kwa ajili ya uamuzi
Nondo awasilisha barua ya kumkataa Hakimu Mpitanjia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment