Huku akikabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, Harbinder
Sing Sethi ameondolewa katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni ya kufua umeme
ya Independent Power Tanzania (IPTL).
Uamuzi wa kumuondoa Seth katika ukurugenzi umefikiwa na bodi
ya wakurugenzi ambayo pia imemvua madaraka ya kuwa mwenyekiti mtendaji wa IPTL,
baada ya kushindwa kushiriki na kuhudhuria mikutano ya bodi
Seth anadaiwa kushindwa kuhudhuria vikao vya bodi bila kuruhusiwa
na wakurugenzi wenzake kwa miezi sita mfululizo tangu Juni 19, 2017
alipokamatwa na kushitakiwa. Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi wa IPTL, Ambroce Lugenge wakati akitoa muhtasari wa
maazimio yao wakati wa mkutano mkuu wa tatu uliofanyika Aprili 10
Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu ya kutafuta ufumbuzi wa
changamoto zinazoikabili kampuni hiyo na uendeshaji wa mambo yanayohusu IPTL
Sethi anakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi,
utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola22.198 milioni za
Marekani na Sh309.5 bilioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu.
“Bodi ilijadili kuhusu kesi namba 27 ya 2017 ya uhujumu
uchumi inayomkabili ndugu Harbinder Sing Sethi na athari yake kwa kampuni,
muundo wa kiutendaji wa kampuni ikiwemo na uongozi, udhibiti na ushushaji wa
gharama pamoja na uwepo wa kesi mbalimbali mahakamani dhidi ya kampuni au ya
kufunguliwa na kampuni,” alisema Lugenge
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilisema
bodi ilimtunuku Sethi ukurugenzi wa heshima kwa msingi kuwa “aliongoza” kampuni
hiyo kutoka katika hatari ya kufilisiwa kutokana na kesi iliyokuwa imefunguliwa
na kampuni ya VIP Engineering and Marketing kati ya mwaka 2002 hadi 2013
Kutokana na uamuzi huo, Sethi hataruhusiwa kwa namna yoyote
ile kushughulikia masuala yanayohusu kampuni hiyo au kuingia makubaliano yoyote
kwa niaba ya kampuni.
“Bodi imeelekeza uongozi mpya, hasa menejimenti kuwafikia
wadau ikiwa ni pamoja na Serikali ili kuangalia namna bora ya kutatua madai
yote dhidi ya kampuni, ikiwemo hasara inayodaiwa kusababishwa na ndugu Sethi
kwa mamlaka husika, iliyopelekea kukamatwa na kushtakiwa kwake ibebwe na
kampuni na kuyatafutia ufumbuzi kwa masilahi ya umma,” alisema Lugenge katika
taarifa hiyo
Pia, alisema bodi imeagiza menejimenti mpya kukaa na Mamlaka
ya Mapato ya Tanzania (TRA) ili kubaini kodi stahiki na kuweka mazingira bora
ya kuzilipa haraka iwezekanavyo baada ya kubaini kiasi kisicho na pingamizi.
Lugenge katika taarifa hiyo alisema bodi hiyo imemteua Joseph Makandege kuwa
mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ili kuongoza uboreshaji kiutendaji, uteuzi
ulioanzia Aprili 10
Alisema katika mkutano, bodi ilijadili na kufikia maazimio
katika vipengele vingine 10 vya ajenda, ambavyo vilikuwa vinachangia kwa kiasi
kikubwa kuamua mwelekeo na hatima ya kampuni hiyo
Sethi avuliwa ukurugenzi wa IPTL akiwa mahabusu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment