Waziri Mkuu kuzindua miradi mikubwa mitatu kesho Lindi


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kutua mkoani Lindi kesho ambapo atazindua mradi wa kuunganisha mkoa huo na wa Mtwara katika gridi ya Taifa

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa leo Mei 20 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Waziri Mkuu

Amesema kwa siku ya kesho, Waziri Mkuu atazindua miradi mikubwa mitatu ukiwamo wa kuunganisha Lindi na Mtwara kwenye gridi ya taifa

Pia Waziri Majaliwa atakagua miundombinu ya uingizaji mafuta katika mkoa huo ambao unatarajia kuanza kupokea mafuta ya petrol na dizeli mwezi ujao

“Atakwenda kujionea miundombinu ya uingizaji mafuta kupitia bandari ya Mtwara, habari njema iliyopo kuanzia Juni utaanza kupokea mafuta kupitia bandari ya Mtwara,” amesema Byakanwa
Amesema Waziri Mkuu atakwenda kwenye uzinduzi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme Mtwara

Pia amesema miundombinu ya Bandari ya Mtwara itakuwa na uwezo wa kupokea lita 25 milioni za mafuta lakini kwa kuanzia Juni wataanza na lita 10 milioni

“Kampuni mbili tayari zimeshaagiza mafuta lita 10 milioni, wafanyabiashara wengine sasa waone Mtwara kama sehemu ya fursa na itapunguza msongamano," amesema.

Waziri Mkuu kuzindua miradi mikubwa mitatu kesho Lindi Waziri Mkuu kuzindua miradi mikubwa mitatu kesho Lindi Reviewed by KUSAGANEWS on May 20, 2018 Rating: 5

No comments: