Viongozi wa dini waaswa kuepuka migogoro


Viongozi wa dini wameaswa kuepuka migogoro ya mara kwa mara katika makanisa yao na badala yake waendelee kuwajenga waumini wao wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa

Pia imesema inawashukuru viongozi wa dini na madhehebu yote ya dini kwa kuendelea kuiombea nchi amani, mshikamano na utulivu, jambo ambalo linaongeza chachu kubwa kufikia mafanikio ya maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ibada ya kutawazwa Askofu Dkt. Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga kuwa Askofu Mkuu wa saba wa Kanisa la Anglikana Tanzania.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma

“Nawaombeni wote kwa ujumla wetu, tuendelee kutumia makanisa yetu kuombea Taifa hili ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano.  Watu wa Mungu ni watu wa upendo, watu wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho,” amesema

Waziri Mkuu ameongeza kuwa: “Haitarajiwi kuona watu wa Mungu wakiwa katika mstari wa mbele kuchochea migogoro, kuvunja amani ya kanisa na kuongoza makundi yanayopingana katika kazi ya Bwana.”

Viongozi wa dini waaswa kuepuka migogoro Viongozi wa dini waaswa kuepuka migogoro Reviewed by KUSAGANEWS on May 20, 2018 Rating: 5

No comments: