Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh.Selemani Jafo
ameikataa taarifa ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa jengo la maabara katika
hospitali ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga kwa ufadhili wa mradi wa boresha
afya USAID baada ya kuelezwa kuwa jengo hilo litagharimu zaidi ya Shilingi
Milioni 990 kwa madai kuwa thamani ya fedha hailingani na uhalisia
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi mji wa
Mafinga mkoani Iringa Waziri Jafo amesema kiasi cha Shilingi Milioni 990
kinatia shaka ikilinganishwa na jengo jingine la vyumba vitatu vya upasuaji
lilojengwa hospitalini hapo kwa Milioni 232 kwa ufadhili wa nchi ya Japani
Jafo pia amemuagiza mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri
Wiliamu kutowapeleka viongozi wa kitaifa katika jengo hilo mpaka watakapo
patiwa thamani halisi kwa kuwa halmashauri imekuwa haishirikishwi katika hatua
mbalimbali za ujenzi
Akiwa mjini Mafinga Jafo amekagua miradi inayoendelea
kujengwa inayopatiwa fedha na wizara ya TAMISEMI ya ujenzi wa mabweni na vyumba
vya madarasa shule ya sekondari Changarawe, ujenzi wa chumba cha upasuaji kituo
cha afya Ihongole na madarasa mabweni na bwalo katika shule ya msingi makalala
ya watoto wenye ulemavu mchanganyiko wanaofikia 554 kwa idadi
Waziri Jafo Atilia shaka thamani ya fedha ujenzi jengo la Maabara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment