Nchi za EAC kuwa na Sheria na sera zenye taf siri moja

Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaohusika na usalama wameazimia kwa pamoja kuwa na sera na sheria zenye tafsiri ya pamoja katika kusimamia baadhi ya masuala yanayohusu usalama wa nchi hizo

Maazimio hayo yamefikiwa jijini Arusha yalipo makao makuu ya EAC na Mawaziri hao katika kikao cha kisekta ambapo kwa upande wa Tanzania waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani Dakta Mwigulu Nchemba anasema miongoni mwa maazimio yaliyopelekwa na Tanzania ni pamoja na kuwa na tafsiri moja kwenye suala la dawa za kulevya.
Kumekua pia na ongezeko la biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, hili nalo limewekwa kwenye maazimio hayo ambayo yanatarajiwa kufikiwa maamuzi kwenye kikao cha wakuu wa nchi mwezi Novemba.



Nchi za EAC kuwa na Sheria na sera zenye taf siri moja Nchi za EAC kuwa na Sheria na sera zenye taf siri moja Reviewed by KUSAGANEWS on May 26, 2018 Rating: 5

No comments: