Ajira za watu zaidi ya 500 katika sekta ya madini ziko
mashakani kupotea kufuatia wamiliki wa viwanda 25 vya kuchenjua na kununua
dhahabu vilivyoko mkoani Mwanza kutishia kuvifunga, baada ya Mkuu wa mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel kuzuia usafirishaji wa malighafi inayotumika
kubebea dhahabu maarufu kama Carbon kutoka Geita kwenda Mwanza mahali vilipo
viwanda hivyo
Wachenjuaji na wanunuzi hao wa dhahabu wamesema hawako
tayari kwenda kuwekeza mkoani Geita ambako hakuna soko la dhahabu na pia kwa
kuhofia usalama wa mitaji yao kwani uwekezaji waliokwisha ufanya katika mkoa wa
Mwanza ni mkubwa unaofikia zaidi ya shilingi Bilioni 15 za Kitanzania.
Kamishna Msaidizi wa madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi
Yahya Semamba naye ameunga mkono agizo la Mkuu wa mkoa wa Geita la
kutosafirisha Carbon kwenye viwanda vya uchenjuaji mkoani Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Aprili 24
mwaka huu alipiga marufuku usafirishaji wa Carbon za mkoa wa Geita kwenda
Mwanza kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu akidai zinaupotezea mkoa wake
asilimia 60 ya mapato ya thamani ya dhahabu inayochimbwa mkoani humo
Ajira za watu zaidi ya 500 katika Sekta ya Madini ziko mashakani.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment