Wakazi wa kijiji cha Mngoji kata ya Madimba mkoani Mtwara
wameiomba serikali na wadau wengine wa mendeleo kusaidia kumalizia ujenzi wa
zahanati ambayo ipo katika hatua za kupaua, ili waondokane na adha ya akina
mama
Wakazi hao wamesema kujengwa kwa zahanati hiyo kutasaidia
wakazi wa kijiji hicho cha Mngoji wapatao 2,800 kupata huduma za afya kwa
karibu zaidi, pamoja na kitongoji cha Uyuvi ambacho kipo umbali wa kilometa 10
toka zahanati ya Madimba
Akikabidhi msaada wa hundi ya mfano ya shilingi Milioni
ishirini na moja laki moja hamsini na moja elfu na mia tano – 21,151,500
kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo kwa mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda ambae
nae aliikabidhi kwa uongozi wa kijiji, meneja wa mawasiliano wa shirika la
maendeleo ya Petrol – TPDC Mariam Mselemu amesema, shirika hilo limetoa msaada
huo katika kutekeleza sera ya uwajibikaji kwa jamii ya kurudisha kidogo
walichonacho kwa jamii.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya Evod Mmanda mbali na kutaka
fedha hizo zitumike kwa makusudi yaliyokusudiwa amewataka wananchi kuwa na
taadhari kubwa ya ugonjwa wa Ebola kwa kuzingatia kijiji hicho cha mngoji ni
miongoni mwa vijiji lilivyopakana na nchi jirani ya msumbiji
Serikali yaombwa kumalizia ujenzi wa zahanat i mkoani Mtwara.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment