Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepiga
marufuku uchinjaji wa mifugo katika machinjio na minada isiyo rasmi ili
kuwalinda walaji na magonjwa ya ulaji wa mifugo isiyopimwa na daktari lakini
pia kuiingizia kipato halmashauri hiyo
Marufuku hiyo impigwa na Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya
wilaya ya Tunduru Dkt. Erick Kaisy aliyemwakilisha Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo kwenye uzinduzi wa awali wa mnada wa mifugo wa halmashauri
hiyo ulioko Muhuwesi wilayani Tunduru unaotarajiwa kusaidia mikoa jirani ya
Lindi na Mtwara.
Kwa upande wao wafugaji wanauzungumzia mnada huo huku
wakiiomba serikali kuendelea kuwaelimisha wafugaji waachane na kuuza Ngo'mbe
zikiwa zizini na badala yake wazilete mnadani.
Nao wafanyabiashara wa nyama ya Ngo'mbe wilayani Tunduru
wanasema kuwa mnada huo utawasaidia kwa kuwa awali walikuwa
wakifuata Ngo'mbe nje ya mkoa wa Ruvuma na hivyo unatarajiwa kusaidia
kupunguza gharama ya nyama
Uchinjaji holela wapigwa marufuku Tunduru
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment