Waziri atatua mgogoro wa ardhi kwa Somji

Serikali imerasimisha eneo la Dovya lililoko Boko kata ya Bunju maarufu kwa Somji lenye ukubwa wa ekari 366 kuwa eneo la makazi.

Akitoa maelezo hayo leo Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi amesema wakazi wote waliovamia eneo hilo mali ya serikali, hawatavunjiwa bali watahakikisha linapimwa na kila mtu analipa kodi

"Nimekuja kumaliza mgogoro eneo hili mali ya serikali niseme wote mliojenga ni wavamizi hamtavunjiwa litapimwa na kila mtu atalipa kodi." Amesema Lukuvi

Amesema eneo hilo lililokuwa mali ya Somji mwaka mpaka 1952, lakini baadaye  serikali ililichukua hilo kwa manufaa ya umma na kutaka kuwapangia wananchi namna ya kuishi ila wananchi walikuwa na haraka na kuvamia eneo hilo

"Serikali ilitaka kuwapangia namna ya kuitumia ardhi hiyo ila nyie mkawa na haraka ya kujipangia nimewahi kuwa mkuu wa mkoa eneo hili nalifahamu lakini leo nimekuja niwaambie ukweli," amesema

Baada ya serikali kumiliki eneo hilo, Somji alifungua kesi akitaka alipwe fidia   mwaka 2010 na Mahakama ilitoa hukumu na kuagiza Somji alipwe fidia na eneo hilo libaki mali ya serikali 
Waziri atatua mgogoro wa ardhi kwa Somji Waziri atatua mgogoro wa ardhi kwa Somji Reviewed by KUSAGANEWS on May 12, 2018 Rating: 5

No comments: