Majaji walazimika kusikiliza kesi kwa muda wa ziada Arusha.

Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, yenye Makao yake Makuu Jijini Arusha wanalazimika kusikiliza  kesi kwa muda wa ziada ili kukamilisha kesi za wananchi wa nchi mbalimbali za Umoja wa Afrika yanayoendelea kuwasilishwa  Mahakamani hapo

Hatua ya majaji hao imeelezwa na baadhi ya wadau wa sheria kuwa ni mfano wa kuigwa

Miongoni mwa kesi zinazoendelea katika Mahakama hiyo ni pamoja na iliyofunguliwa na raia wa Ivory Coast anayeilalamikia Mahakama Kuu ya Tanzania, raia wa Ghana na raia wa Benin wote wakiwa wana lala mikia ukiukwaji wa haki zao uliofanywa na  Mahakama za nchi zao wakati wa kusikiliza mashtaka yaliyokuwa yanawakabili

Katika kesi ya raia wa Ivory Coast aliyepatikana na hatia ya mauaji ya mke wake anayeishtaki Mahakama Kuu ya Tanzania, amelalamika kuwa wakati kesi yake ina endeshwa hakupata msaada wa sheria.
Pia Wakili wa raia huy amelalamikakuwa mteja wake hakuwa anaelewa Kiswahili na Kingereza zilizokuwa zinatumika jambo  lililosababisha ashindwe kuelewa kilichokuwa kinazungumzwa malalamiko ambayo pia yametolewa na ya raia wa Ghana na pia wa Benin



Majaji walazimika kusikiliza kesi kwa muda wa ziada Arusha. Majaji walazimika kusikiliza kesi kwa muda wa ziada Arusha. Reviewed by KUSAGANEWS on May 12, 2018 Rating: 5

No comments: