|
Wananchi katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamejenga zahanati katika vijiji 33 kwa nguvu
zao ili kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu wa kutafuta huduma za
matibabu.
Kwa upande wa serikali imesaidia
kununua vifaa vya viwandani kukamilisha zahanati hizo
|
|
|
Wananchi hao wamesema wameamua
kujenga zahanati baada ya kuchoshwa na adha ya muda mrefu ya kutafuta huduma
za matibabu mbali hali inayosababisha vifo vya wajawazito na watoto vijijini
|
|
|
Afisa Mipango wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mbinga, Bwana BRUNO MAPUNDA amesema wameguswa na jitihada za
wananchi na kuamua kuagiza vifaa kutoka viwandani kwa bei nafuu ili
kukamilisha zahanati zilizojengwa na wananchi
|
|
|
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Bwana GOMBO SAMANDITO GOMBO
amesea kwa kushirikiana na wananchi ni azma yake kujenga zahanati katika
vijiji vyote vya halmashauri hiyo ili kutimiza mpango wa serikali wa kila
kijiji kuwa na zahanati
|
|
Wananchi wajenga zahanati katika vijiji 33 wilayani Mbinga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment