Zikiwa zimepita siku tatu tangu Serikali ilipowaagiza
wafanyabiashara wa mafuta ya uto (kula) kuanza kuyaingiza sokoni, hali ya
upatikanaji wake siyo nzuri kutokana na kuendelea kupanda bei jijini Dar es
Salaam.
|
|
Leo ndiyo siku ya mwisho tangu Serikali ilipotoa amri hiyo na
kuanzia kesho huenda msako katika bohari na maghala ya wafanyabiashara hao
ukaanza
Akizungumza bungeni juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa
muda wa hadi leo kwa wamiliki hao kuingiza sokoni bidhaa hiyo na kuonya kuwa
iwapo hilo halitafanyika Serikali itaanza msako hu
Jana, Mwananchi lilipita katika maeneo mbalimbali ya
wafanyabiashara wa mafuta wa jumla na rejareja jijini Dar es Salaam ambap wengine walisema wamelazimika kuacha kuyauza na wale wanaoendelea nayo
wamekuwa wakiyauza kwa bei ya juu
Wale wanaositisha uuzaji huo walisema wanafanya hivyo kutokana na hofu ya kukosa wateja kutokana na kuuziwa kwa bei ya juu na wauzaji
wakubwa itakayowalazimu na wao kupandisha bei
“Sijaweka mafuta ya uto hapa kwangu hii ni wiki sasa, hapo awali
nilikuwa ninanunua dumu la lita 20 Sh54,000 ghafla ikapanda hadi Sh56,000 nikaamua kuacha kwa sababu nawafahamu wateja wa mtaa huu nikipandisha bei hawatanunua,” alisema Joyce Pius, mmoja wa wafanyabiashara hao.
Joyce alisema kutokana na kutouza mafuta hayo dukani kwake
anakosa wateja wa bidhaa nyingine kama vile unga wa sembe, ngano, mchele na
sukari
Mfanyabiashara wa duka la jumla katika eneo maarufu la Kinondoni
TX, Ally Salim alisema wakati mafuta yanapanda alikuwa na akiba ya kutosha
kwenye ghala lao
Aliongeza kuwa kwa sasa wananunua lita 10 ya mafuta hayo kwa
Sh38,000 na kulazimika kuuza kwa kati ya Sh40,000 hadi Sh42,000 kulingana na
umbali wanakoyanunua
Mfanyabiashara wa duka la rejareja katika Kata ya Mzimuni, Lucy
Lazaro alisema, “Nimenunua leo dumu la lita 20 kwa Sh64,000 kutoka Sh54,000
niliyonunua mwishoni mwa wiki iliyopita
“Tunalazimika kuuza chupa ya lita moja kwa Sh3500 hadi Sh400
kutoka Sh3200 ya awali na bado inakata. Hili dumu la lita 20 lina chupa za
lita moja 20 tu, ukijumlisha kumwagika na kuwaongeza kidogo wateja unajikuta
unabaki na chupa 18 na nusu au 19, hivyo ni hasara tu.”
Katika eneo la Temeke, mafuta ya kula nusu chupa yaliyokuwa
yakiuzwa Sh500 sasa yanauzwa Sh700
Mchuuzi wa mafuta na bidhaa nyingine katika eneo la Tandika
Azimio, Abdul Hafidh alisema anafanya biashara hiyo kwa mazoea. “Kupitia
mafuta nitauza unga wa ngano na dengu, mchele na sukari kwa sababu wateja
wangu ni wauzaji wa vitumbua na mama lishe, hivyo nisipokuwa na mafuta ya
kula na walizoa kununua hapa nitawapoteza, ”alisema Hafidh
Gazeti hili jana lilifika katika ofisi za kampuni Murzah Oil
Mills zilizopo eneo la Kipawa kutaka kujua kama agizo la Waziri Mkuu limeanza
kutekelezwa, lakini lilipokewa na walinzi waliolekeza kuonana na ofisa mmoja
aliyetoa maelezo kuwa si msemaji na kutaka atafutwe msemaji ambaye ilielezwa
yupo katika ofisi nyingine zilipo eneo la Masaki
“Naomba chukua namba hii ya msaidizi wake (wa bosi) ili
uzungumze naye,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka kujitambulisha
Hata hivyo, alipopigiwa msaidizi huyo alipokea na kutaka apewe
muda ili awasiliane na bosi wake na kuahidi kutoa majibu baadaye. Hata hivyo,
alipotafutwa tena simu yake iliita bila majibu yoyote
Juhudi za kuwapata wasambazaji wengine wakubwa wa mafuta
hazikuzaa matunda
|
Mafuta ya kula Dar bado kizungumkuti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment