Walimu mkoani Mwanza
wamesema iwapo mkurugenzi wa halmashauri zao hawatawalipa pesa zao za uhamisho,
wataandamana mpaka kwa Waziri Mkuu au kwa Rais, ili kupeleka malalamiko yao.
Akizungumza mbele ya wandishi wa
habari mmoja wa walimu walioandamana mkoani Mwanza kudai stahiki zao za
uhamisho, Mwl. Anicet Majira wa shule ya sekondari Njolay, amesema iwapo
hawatalipwa haki zao watalazimika kuendeleza maandamano hayo, licha ya usumbufu
mkubwa wanaopata.
“Msimamo wetu ni mmoja, kama leo
Rasi alivyolega lega na Mkuu wa Mkoa akashindwa kulitatua hili, moja kwa moja
tutakwenda kwa waziri husika, kama waziri husika atashindwa tutakwenda kwa
Waziri Mkuu mpaka kwa Rais, kwa hiyo msiamamo wetu ni sisi kulipwa kilicho
chetu”, amesema Mwalimu huyo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
John Mongela, amewataka walimu hao kuwa na subira mpaka tarehe 24 May, ili
walitafutie suluhu jambo lao.
Walimu mkoani Mwanza wamendamana leo
hii hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kudai pesa zao uhamisho, kama serikali
inavyotaka
"Tutaandamana mpaka kwa Rais" – Walimu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 12, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment