Profesa Shivji: Kazi ya uanahabari ni kazi takatifu

Mgeni rasmi katika tuzo za umahiri wa habari zinazotolewa na Baraza la Habari nchini (MCT)Profesa Issa Shivji amesema kazi ya uandishi wa habari, ni kazi takatifu

Shivji ambaye pia ni Mwanasheria na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameyasema hayo leo Mei 12, katika utoaji wa tuzo za umahiri wa habari za Ejat

“Nyie kazi yenu ni kuwezesha umma kufurahia haki na uhuru. Ninadiriki kusema kazi yenu ni kazi takatifu nasema kwa dhati kabisa,” amesema

Shivji amesema anawapongeza wanahabari kwa kazi wanayofanya hasa katika kipindi hiki kigumu

“Ugumu wa kazi yenu unajulikana,” amesema Profesa Shivji
Profesa Shivji: Kazi ya uanahabari ni kazi takatifu Profesa Shivji: Kazi ya uanahabari ni kazi takatifu Reviewed by KUSAGANEWS on May 12, 2018 Rating: 5

No comments: