Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga
amefunguka na kumuomba radhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya watu wa
Iringa kwa kukosa kura 25 za udhamini katika kipindi cha kampeni za uchaguzi
2015.
Balozi Maiga amesema hayo leo Mei 1,
2018 kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa
inafanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
ni Kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya
wafanyakazi"
"Nakumbuka Mhe. Rais ulipata
shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini ikabidi utoke nje ya mji ndiyo
ukapata, ila wadhamini 25 kwa hapa mjini kura hazikupatikani tunakuomba radhi
sana Mhe. Rais kwa kukosa busara hiyo lakini ulipokuwa hapa ulitoa ahadi kwa
wana Iringa na umezitimiza, ahadi ya kwanza ulisema Iringa itakuwa Makao Makuu
ya Utalii ya mikoa ya kusini hilo tumeshalifanya, Mkuu wa mkoa aliitisha vikao
na watu wa mikoa mingine lakini hasa wewe umeshafanya maamuzi kuwa Uwanja wa
ndege wa Iringa wa Nduli utarekebishwa na kuweza kuchukua ndege kubwa zaidi
kama zile za Bombidier"
Aidha Maiga aliendelea kusema
kuwa
"Na
umeshachukua maamuzi kwamba barabara ya kutoka hapa Iringa kwenda hifadhi ya
Ruaha itakuwa katika kiwango cha lami mara nyingi na mimi nimekuwa nakuomba na
kukukumbusha kuhusu maendeleo ya mkoa wa Iringa, umenisikiliza na kutekeleza
hapa Iringa pekee yake mjini barabara zimetengenezwa kwa kutumia bilioni 6.4,
shule kongwe kwama vile Tosamaganga, Malangali zimeboreshwa, miradi ya afya na
maji ni mabilioni siwezi kusema lakini kubwa kabla ya kufika hapa umefungua
barabara kuu ya Afrika ya Kati na Afrika Mashariki, barabara hii inapita
katikati ya mkoa wa Iringa juzi pale Isimani umesema barabara hii iwe mkombozi
kwa watu wa Iringa"
Waziri amwomba radhi Magufuli kukosa kura 2015
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment