Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi
wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kunyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).
Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji
hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na
baadae kufariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,
Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea
katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.
Katika tukio hilo polisi walifanya
uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta
mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu
marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa
hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi
ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Amuuwa mpenzi wake kwa kumnyonga shingo, Mwanza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment