Msanii wa filamu bongo
Mzee Majuto leo Mei 1, 2018 anatarajiwa kusafiri na kwenda nchini India kwa
ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita.
Steve Nyerere ambaye amehusika kwa
namna moja au nyingine katika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee
Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo
Mzee huyo atakwenda kwa matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao
wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.
"Niseme ahsante sana Mhe. Rais
John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy Mwalimu na wadau pamoja na wasanii
mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa
njiani kwenda India kwa matibabu zaidi"
Steve Nyerere hakuishia hapo
alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto
kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na bima ya afya na kusema ni mkombozi kwao,
anadai haiwezekani miaka nenda rudi wakawa ni watu wa kuombaomba kila wakati
pindi wanapopata matatizo ili hali wanapata pesa za kutosha.
"Tuna kuombea kwa namna moja
ama nyingine ,Baba naamini kwa maombi ya Watanzania utarudi katika kazi za
ujenzi wa Taifa lako,Kuinua sanaa yetu,Kupeperusha bendera ya mkoa wako ,Baba
kuumwa kwako kuna mafunzo mengi kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla wake,
Wasanii wenzangu bima ya afya ni kitu muhimu kwako na kwa familia yako, Bima ya
Afya ni mwokozi kwetu. Sidhani kama miaka nenda rudi tutakuwa watu wa kuomba
msaada ,tujiulize tunafanya mapart, tunakunywa na kusaza ,tunajinadi kwenye
mitandao nguo zetu kuanzia milioni 3 mpaka 4 tukiulizwa umejipangaje kwa kesho
amna kitu, ni muda wa kuamka sasa ,naamini majukumu hayakimbiliki bali
tunayakabili" alisisitiza
Steve Nyererere
Mzee Majuto kupelekwa India leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment