Familia ya marehemu, Suguta Chacha imesema mazishi ya ndugu
yao yatafanyika Alhamisi ya Mei 3, 2018 kijiji cha Nyabitocho
Chacha alifariki mikononi mwa Polisi, usiku wa Aprili 27
mwaka huu
Akizungumza leo Mei Mosi, na waandishi wa habari katika
kijiji cha Nyabitocho kata ya Mbogi wilayani hapa, mbunge wa jimbo la Tarime
Vijijini, John Heche ambaye ni kaka wa marehemu alisema uamuzi wa familia
kuzika mwili huo umekuja baada ya kuridhika na hatua za serikali katika tukio
hilo
"Tumeridhika na hatua zilizochukuliwa na jeshi la
polisi kwa kumtia hatiani mtuhumiwa, kumfikisha mahakamani na kusomewa shtaka
la kuua, kama familia tumeona ni vyema tuutangazie umma kuwa kesho tutauchukua
mwili wa marehemu na kuuleta nyumbani na kesho kutwa (Alhamisi Mei 3)
tutamzika." amesema Heche
Familia yataja tarehe ya mazishi ya aliyeuawa na polisi Tarime
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment