Kenya. Rais
Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya asilimia tano kwa kiwango cha chini cha
mshahara nchini Kenya.Huku akisisitiza uwepo wa mazungumzo kutatua migogoro ya
migomo
Nyongeza hiyo
ya mishahara imetangazwa na Waziri wa Kazi Balozi Ukur Yatani Kanacho
aliyemwakilisha Rais Kenyatta wakati wa maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi duniani
Maadhimisho
hayo ambayo yamefanyika kwenye viwanja Uhuru Park pia yamehudhuriwa na viongozi
wengine mashuhuri kutoka serikalini
Mwaka 2017
Rais Kenyatta alihudhuria na kuhutubia taifa lakini mwaka huu 2018 mambo
yamekuwa tofauti ambapo Waziri Yatani ndiye amemwakilisha kiongozi huyo
Kwa mujibu wa
hotuba ya Rais iliyosomwa na waziri huyo, Serikali imetangaza
kuwaongezea watumishi wa umma nyongeza ya asilimia tano ya mshahara.
Hotuba hiyo imelenga mambo manne
yakiwamo kuangazia usalama wa chakula nchini, makazi bora na nafuu,
ujenzi wa viwanda ili kukabiliana na ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, na
matibabu bora
Kenyatta mwaka
2017 alitangaza nyongeza ya asilimia 18 kwa wafanyakazi wa umma
Hata hivyo,
Katibu Mkuu wa Cotu Francis Atwoli amesema agizo hilo halijatekelezwa kwa
baadhi ya kampuni na taasisi
"Kuna
kampuni nyingi hazijatekeleza agizo hilo. Rais pia alipendekeza ushuru kwa
wanaopokea mshahara wa chini ya Sh100,000 upunguzwe lakini hayo yote
hayajazingatiwa," amesema Atwoli
Kiongozi wa
upinzani Raila Odinga aliyehudhuria maadhimisho hayo, amesema
mkataba wa salamu zake na Rais Uhuru Kenyatta wa Machi 2018, ulilenga
kuimarisha maisha ya Wakenya
"Mazungumzo
yetu yaliegemea kuimarisha maisha ya wananchi wote, kwa msingi wa bidhaa na
kodi nafuu ya nyumba," amesema Odinga
Ameongeza
kuwa Nasa imeungana na Serikali ya Jubilee ili kuangazia matatizo yanayowakumba
Wakenya ikiwamo kukabiliana na kero za ufisadi
Wengine
waliohudhuria maadhimisho hayo ni; Waziri wa Elimu Amina Mohamed, Waziri wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Peter Kimunya, Musalia Mudavadi, Seneta
wa Nairobi Johnson Sakaja, Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Nairobi
Esther Passaris, mbunge maalum wa ODM na katibu wa KNUT Wilson Sossion na
viongozi wengine mashuhuri serikalini.
Kenyatta aongeza mishahara Kenya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment