Mamlaka ya
Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya
wastani, kwa siku tano zinazoweza kusababisha mafuriko katika maeneo mengi
nchini
Kwa mujibu wa
TMA, mvua hizo zitaanza leo Mei Mosi mpaka Mei 5 mwaka huu na zinatarajiwa
kunyesha mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na
Pemba
Mikoa mingine
ni Mara, Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi,
Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara
TMA imesema
kiwango cha athari zinazoweza kutokea katika jamii ni pamoja na adha ya
usafiri, barabara kubwa kutopitika na maji kujaa au kupita kwa kasi
Pia imetoa
wito kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea
kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.
TMA yatoa tahadhari ya mvua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment