Mamlaka ya
Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta ya
petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa asilimia 0.9 hadi asilimia 3.8 kuanzia
kesho, Mei 2
Taarifa
iliyotolewa leo Mei Mosi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany
amesema bei hiyo ni kwa upande wa Tanzania bara
Hata hivyo, punguzo
hilo ni kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika bandari ya Dar es Salaam
huku watumiaji wa bandari ya Tanga bei ikiongezeka
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo ikilinganishwa na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4, bei ya
petroli imepungua kwa Sh88 kwa lita (asilimia 3.8) na dizeli Sh61 kwa lita
(asilimia 2.75) huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Sh2 kwa lita sawa na
asilimia 0.09
Kadhalika bei
ya wanunuzi wa jumla wa bidhaa za petroli nayo imepungua kwa Sh100.91 kwa lita
(asilimia 4.58), dizeli Sh73.71 kwa lita (asilimia 3.52) na mafuta ya taa ni
Sh10.49 kwa lita sawa na asilimia 0.51
Mafuta
yanayopita bandari ya Tanga bei yake kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka kwa
asilimia 0.14 kwa petroli na asilimia 0.71kwa dizeli lakini wauzaji wa jumla
bei imepungua kwa asilimia 0.46 (Sh9.8 kwa lita) kwa petroli na asilimia 0.1
(Sh1.9 kwa lita) kwa dizeli.
“Hakuna uingizaji mpya wa mafuta uliofanyika
nchini kupitia bandari ya Tanga lakini kutokana na mabadiliko ya bei ya Ewura
lakini kuna mabadiliko ya bidhaa hizo tofauti na ilivyotangazwa Aprili 4. Bei
ya petrol itaongezeka kwa sh3 kwa lita huku dizeli ikiongezeka kwa Sh15 kwa
lita,” imeeleza taarifa hiyo
Kutokana na
kupungua kwa mafuta ya taa katika bandari, watumiaji wa mafuta ya taa wa mikoa
ya nyanda za juu ambao hutumia bandari hiyo, wameshauriwa kuchukua bidhaa hiyo
katika bandari ya Dar es Salaam kwa bei elekezi.
Ewura yashusha bei ya dizeli, petroli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment