Rais John Pombe Magufuli
ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa Iringa pamoja na RPC mkoani humo kumpatia msaada
mwanamama Salmakoni Sanga ikiwa ni pamoja na kumpima kama kweli ametolewa
kizazi baada ya kudai kushambuliwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Mussa.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo
baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe za Mei Mosi mkoani Iringa ambapo
mama huyo alijitokeza na kumlilia Rais Magufuli ampatie msaada kutokana na
kunyimwa haki yake mahakamani.
Mama huyo amesema kwamba tukio lake
la kushambuliwa na Bw. Mussa lilifanyika mwaka jana ambapo shambulio lilimfanya
apoteze kiumbe kilichopo tumboni hali iliyompelekea kutolewa kizazi.
Hata hivyo mama huyo amesema kwamba
pamoja na maumivu aliyosababishiwa na kijana huyo, bado mahakama ilimuachia
huru mtu huyo na yeye akiamini kwamba alidhulumiwa haki yake na mahakama ya
mkoa huo.
Akitoa maagizo, Rais Magufuli
amemtaka RPC Iringa Juma Bwire na Mkuu wa Mkoa Bi. Amina Masenza kumtafuta
kijana huyo na kumfungulia mashtaka upya hata kama alishinda kesi.
JPM ataka aliyemlilia apimwe kizazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment