Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, kuwashughulikia viongozi wanaowahamisha watumishi wa Umma bila
kuwalipa stahiki zao.
Akiongea leo kwenye maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), mkoani Iringa Rais Magufuli amesema jambo la
kuhamisha wafanyakazi bila kuwalipa ameshapiga marufuku hivyo kama kuna
kiongozi bado anafanya hivyo ni lazima ashugulikiwe.
''Kama patakuwepo na Mkurugenzi ama
kiongozi yoyote anamuhamisha mfanyakazi, awe mwalimu au mtumishi yoyote bila
kumlipa posho yake ya uhamisho na wawe bado wanaendelea kufanyakazi, Mh. Waziri
Mkuu lisimamie hilo wao wahame moja kwa moja kwenye kazi zao'', amesema.
Awali Risala ya Chama Cha
Wafanyakazi nchini TUCTA ilieleza pamoja na kuwepo kwa zuio hilo la Rais,
lakini bado wafanyakazi wanahamishwa bila kulipwa stahiki zao jambo ambalo ni
kinyume na taratibu za kazi.
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa
ikitokea kiongozi anamuhamisha mfanyakazi lazima amlipe stahiki zake kwanza
vinginevyo huyo kiongozi ni jeuri na dawa yake ni kumuondoa hivyo Mawaziri
wanaohusika walifanyie kazi hilo.
Rais Magufuli atoa agizo kwa Waziri Mkuu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment