Mwakilishi wa Jimbo la
Paje, Jaku Hashim Ayoub ameitaka serikali kuchukua hatua za kuwadhibiti waajiri
wanaojihusisha na vitendo vya kuwaomba wanawake rushwa ya ngono kwenye ajira.
Mwakilishi huyo ameyasema hayo
katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akiuliza swali lake la msingi
kuhusu wanawake kudaiwa rushwa ya ngono na wanatakiwa wafanye nini wanapokutana
na kadhia hiyo.
Akijibu swali la hilo, Naibu Waziri
wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Shadia Mohammed amesema
serikali haina takwimu za matukio hayo kwa kuwa wanawake wengi hawaelewi rushwa
ya ngono ila viashira huwa vinaonekana na hushindwa kuripoti vitendo hivyo.
"Wanawake wanashindwa kuripoti
matukio hayo kwa kuwa wanahofia kuachishwa kazi au kukosa kazi, kwa kawaida
rushwa ya ngono hufanyika kwa siri sana tofauti na rushwa nyingine na hufanywa
kwa lengo la kupandishwa cheo, mshahara au msaada wowote katika
kazi", amesema Shadia.
Aidha, Shadia amesema serikali
inaendelea kutoa elimu ya rushwa ili kujenga uelewa wa dhana na maana halisi ya
rushwa na kuepukana na matendo hayo.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri
huyo amewataka wanawake wanaokumbana na kadhia hiyo kuenda kuripoti Polisi
pamoja na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa Zanzibar ili kudhibiti matukio hayo.
"Wanawake hawaelewi rushwa ya ngono"- Mbunge Ayoub
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment