Mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la Omari Matonya anatafutwa na jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa
tuhuma za kuwaua kwa kuwachinja mke wake na mtoto wao, kisha kukimbia.
Akizungumza kamanda wa Polisi mkoa
wa Tabora Wilbroad Mutafungwa amesema kwamba mtu huyo amefanya tukio hilo
nyakati za usiku wakati wakiwa wamelala, huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni
wivu wa kimapenzi.
“Mwanamke ambaye anaitwa Moshi Daudi
mwenye miaka 24 akiwa na mtoto wake wa mwaka mmoja anayeitwa Omari Matonya,
waliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mwanaume anaitwa
Omari Matonya mwenye miaka 25, ambaye ni mume wa huyo mama na baba mzazi wa
huyo mtoto, baada ya kufanya tukio hilo alitoweka. Alifanya tukio hilo wakati
familia yake ikiwa imelala na chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi, ambapo
huyo marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa na mahusiano na shemeji yake, ambaye ni
ndugu yake huyo Matonya anayeitwa Lazima Matonya”, amesema Kamanda Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amesema mpaka
sasa hajapata taarfa zake zozote na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta, ili
afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Amchinja mke na mtoto wake wa mwaka mmoja
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment