Mbunge wa Bunda mjini
(CHADEMA) Ester Bulaya amesema Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limefirisika
kutokana na mzigo mkubwa wa madeni ambayo yanaongezeka kila baada ya mwaka na
hivyo kupelekea shirika hilo kujiendesha kihasara.
Mbunge huyo amesema hayo leo Mei 24,
2018, Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia hoja Wizara ya Nishati kwa mwaka
wa fedha 2018/2019 na kusema kuwa kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi
mkuu wa hesabu za serikali deni hilo limeongezeka kwa asilimia 23 mpaka kufikia
mwaka 2015.
“Ukiangalia ripoti ya CAG
imesema kabisa madeni hayana uwiano kati ya mali za shirika la TANESCO na
madeni, kwa namna nyingine TANESCO imefirisika, hili shirika ni wakati muafaka
sasa likagawanywa yakawa mashirika mawili likawa linadeal masula ya uendeshaji
na uzalishaji, Dunia nzima inafanya (hivyo)” amesema Bulaya
Bulaya ameongeza kwamba kama
serikali ina lengo la kujenga Tanzania ya viwanda basi viongozi wanapaswa
kuandaa mipango mizuri ya uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini.
Bunge kwa sasa linachangia hoja
mjadala wa Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Waziri Dkt. Medadi
Kalemani ameomba wabunge kuizinisha jumla ya shilingi trilioni 1.69 ambapo
shilingi trilioni 1.66 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na bilioni 27.1 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida.
“Tanesco imefirisika”- Ester Bulaya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment