Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi imesema imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani
ikiwemo kutofautisha faini wanatozwa waendesha pikipiki kuwa tofauti na zile
zinapigwa za mabasi ya abiria na magari mengine tofauti ya usafirishaji.
Akizungumza leo Bungeni Mjini
Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa
wakati mwingine ajali za kizembe zinatokea kwa waendesha bodaboda kutokana na
kukimbia kutozwa faini kubwa kuliko wa uhalisia wa vyombo wanavyoviendesha.
"Lengo za faini hizo zitakua ni
kwa ajili ya kutoa onyo kwa waendesha vyombo hivyo vya moto ambao takwimu
zinaonyesha kwa sasa ndio wanasababisha ajali nyingi zaidi ambazo zinapelekea
madhara kwa binadamu lakini pia wengi kuacha pikipiki vituo vya polisi kutokana
na kushindwa kulipa faini hizo", amesema Mwigulu.
Msikilize hapa chini Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akielezea zaidi.
Serikali kubadilisha faini za barabarani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment