Wanawake 40 wa ISIS kunyongwa


Serikali inatarajia kuwanyonga wachumba 40 wa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) kulipiza kisasi kwa wapiganaji hao wa jihadi kuikalia kwa miaka mitatu ardhi ya Iraq wakati wa mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kuuawa kikatili

Wanawake hao ambao ni wa kigeni walikiri mahakamani kwamba na wao ni waathirika wa IS, walipewa dakika 10 kila mmoja kutetea uhai wao kabla ya majaji kufikia uamuzi wapewe adhabu kali

Wanawake hao walishutumiwa na mahakama ya Iraq na raia wa kawaida kwa kuwapa msaada waume zao wapiganaji waliosababisha maafa katika eneo walilokuwa wanakalia kuanzia mwaka 2014 hadi 2017

Utetezi wa wanawake

Mwanamke mmoja mwenye uraia wa Ufaransa aitwaye Djamila Boutoutao, 29, alidai kuwa alidhani alikuwa anaolewa na mwanamuziki wa miondoko ya rap

“Ni baada ya kuwasili Uturuki kwa ajili ya ‘mapumziko’ ya wiki moja ndipo nilipogundua ya kuwa mume wangu ni mpiganaji wa kijihadi,” alisema Djamila.

 “Mimi ni mwathirika. Mume wangu alinipiga na kunifungia kwenye pango na watoto wangu nilipokataa kumfuata (hadi Iraq).’

Djamila ni mmoja wa raia wa Ufaransa wapatao 1,900 na wasafiri wa kigeni wanaokadiriwa kuwa 40,000 waliosafiri hadi Syria na Iraq kujiunga na miliki ya khalifa

Uchunguzi wa gazeti
Katika hukumu yake ya hivi karibuni, ambako aliomba asitenganishwe na binti yake, Djamila aliwaambia waandishi wa habari wa gazeti la The Guardian: “Nachanganyikiwa hapa. Nakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha jela maisha. Hakuna anayeniambia chochote, si balozi wetu wala watu ndani ya gereza.”

“Jamani nawasihi msiwaache waondoke na binti yangu. Niko tayari kuwapa fedha endapo mtawasiliana na wazazi wangu. Tafadhali niokoeni.”

Takriban wanawake 40 ndio wamehukumiwa kifo na watu wengine 300 wenye mafungamano na IS wameshauawa

Wanawake 40 wa ISIS kunyongwa Wanawake 40 wa ISIS kunyongwa Reviewed by KUSAGANEWS on May 23, 2018 Rating: 5

No comments: