Walimu watakiwa kuondoa hofu


Walimu waliotoka shule za sekondari na kwenda kufundisha msingi wametakiwa kutokuwa na hofu kwa kuwa hakuna aliyeshushwa cheo na wachukulie ni kama mabadiliko ya kawaida ya kituo cha kazi

Hayo yamesemwa leo Mei 19 na Ofisa elimu mkoa  wa Dar es Salaam, Hamisi Lissu alipokuwa akifunga mafunzo ya kuwaweka sawa walimu wa shule za sekondari wanaoenda kufundisha shule za msingi masomo ya sanaa

“Pamoja na changamoto mnazokumbana nazo hamtakiwi kuwa na hofu kwani mabadiliko mnayokutana nayo ni yakawaida kama kubadili kituo cha kazi,”amesema Lissu

Amesema hamasa imeongezeka na hicho ni kiashirio tosha cha utendaji wao na atahakikisha anatembelea vituo vyao ili kujua changamoto zao kwa kuwa wamekubali agizo la serikali

Kwa upande wake, Meneja mafunzo ya muda mfupi (Aden) Bungendi Joseph amesema walimu wanaotoka sekondari kwenda msingi wanakumbana na changamoto ikiwemo kubadilika kwa lugha,mazingira ya kazi pamoja kubadilika kwa mitaala

“Walimu hawa mazingira wanayoenda ni tofauti hivyo tunawafundisha mazingira ya kulea watoto,namna ya kufundisha lakini kikubwa ni mitaala inayojali umahiri”amesema Bungendi
Advelina Semakamba, Mwalimu wa Sekondari anayekwenda kufundisha shule ya msingi, amesema alipopata taarifa alishtuka lakini baada ya kupata mafunzo ana imani atakwenda kumudu kufundisha

Walimu watakiwa kuondoa hofu Walimu watakiwa kuondoa hofu Reviewed by KUSAGANEWS on May 19, 2018 Rating: 5

No comments: