UONGOZI
wa serikali ya kijiji cha Tumati, umevunjwa kutokana na kusababisha migogoro
kati yao na wananchi kwa miaka minne sasa
Uamuzi wa kuvunja uongozi huo, ulitolewa na mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga, katika mkutano wake alioufanya kijijini hapo juzi
Uamuzi wa kuvunja uongozi huo, ulitolewa na mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga, katika mkutano wake alioufanya kijijini hapo juzi
|
Serikali ya kijiji hicho
ilikuwa ikiongozwa na mwenyekiti Ezekiel Martin (Chadema), lakini tangu mwaka
2015, kumekuwa na migogoro isiyoisha kati ya viongozi na wananchi.
|
|
Baada ya kuvunja uongozi,
Mofuga, alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu,
Hudson Kamoga, kuitisha upya uchaguzi wa kijiji hicho.
|
Alisema hawezi kukubali
kuona wananchi wanalalamikia serikali ya kijiji inayoongozwa na mwenyekiti
wao naye asichukue hatua kwa faida ya jamii.
“Malalamiko mengi
yametolewa na wananchi dhidi ya viongozi wao wakisema wanasababisha migogoro
kila wakati, ni heri waondoke ili wachaguliwe viongozi wengine,” alisema.
Alisema wananchi
wanahitaji viongozi ambao watawaongoza ili wapate maendeleo na siyo kupewa
vitisho na kuibua migogoro.
“Wakae pembeni na
kuwapisha wengine, kwa kuwa wameshindwa kazi,” alisema.
Mapema katika mkutano huo
baadhi ya wananchi waliwalalamikia viongozi wa kijiji hicho kuwa
wanawanyanyasa kupitia uongozi wao hivyo kuwataka waondoke madarakani.
Mkazi wa kijiji hicho,
Elias Boay alisema, viongozi hao wamekuwa wakiwanyanyasa wananchi na kuongoza
kibabe.
"Katika kijiji chetu
hakuna utawala bora unaofanyika zaidi ya udikteta kwani uongozi umekuwa
ukiwaweka rumande baadhi ya wananchi chumba kimoja bila kujali jinsia yao,”
alisema.
Alisema uongozi huo
ulikuwa hausikilizi kero za wananchi na wajumbe wa serikali ya Kijiji
walikuwa wanawatoza watu faini bila kutoa risiti.
Mkazi mwingine, Magdalena
Ombay, alisema iwapo mkurugenzi wa halmashauri ataitisha uchaguzi mwingine,
wanatarajia kuchagua viongozi bora watakaowaongoza vyema na kuachana na
kelele za kila siku.
Hata hivyo, kwa upande
wake, mwenyekiti wa kijiji hicho, Martin alisema, kuvunjwa kwa uongozi wake,
kumetokana na siasa na siyo kwa sababu ya utendaji wao kuwa mbaya.
“Siasa zimeingizwa katika
hili suala kwa sababu ya itikadi ya Chadema niliyonayo.
"Hii mizengwe
ilikuwa tangu siku nyingi hata Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti,
alipofanya ziara yake Mbulu na kufika hapa kijijini baadhi ya watu walimwambia
majungu," alisema.</p>
Dc Mbulu atimua uongozi wa Chadema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment