|
Kongamano hilo lililoongozwa na
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, lilihudhuriwa na Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa Somalia Hassan Sheikh
Mohamud na washiriki wengine kutoka taasisi za kitaifa, kikanda na
kimataifa zinazojihusisha na masula ya usalama na kulinda amani
|
Akisoma mazimio hayo
jana jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa chuo cha Uongozi, Gerase Kamugisha,
alitaja maazimio hayo kuwa ni kuimarisha taasisi za kanda na Umoja wa Afrika
zenye kumu la kujenga na kulinda amani.
|
Alitaja aazimio lingine kuwa ni
kuongeza uratibu, ushirikiano na mashauriano miongoni mwa taasisi za kitaifa,
kikanda na bara zima zinazohusika na juhudi za kuzuia migogoro au kulinda
amani ikiwamo kuimarisha mifumo ya ushirikiano baina ya Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika (AU) na Baraza la Umoja wa Mataifa ili kuongeza
sauti ya Afrika katika maamuzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu amani na usalama wa
Afrika
|
|
Mengine ni kuhakikisha nchi zote
wanachama wa Umoja wa Afrika zinajiunga na kutumia mfumo wa kujitathmini wa
Afrika (APRM) kama chombo muhimu cha kuimarisha maridhiano ya kitaifa na
kuzuia migogoro, uvunjifu wa amani na kuhamasisha serikali kushiriki
kugharamia shughuli za kulinda amani
|
|
Kamugisha alisema kongamano la
kikanda la viongozi wastaafu wa Afrika kuhusu nafasi ya Afrika katika mfumo
wa amani na usalama ulimwenguni lilifanyika Mei 17, mwaka huu jijini
|
|
Alisema kongamano hilo ni
mwendelezo wa kongamano ambalo lilifanyika Johannesburg, Afrika kusini Agosti
mwaka jana
|
|
“Katika kongamano hilo,
viongozi walianzimia kuendeleza mjadala wao kwa kuangalia kwa kina zaidi
suala la nafasi ya Afrika katika mifumo ya usimamizi wa amani na usalama
ulimwenguni,” alisema
|
|
Aidha, alisema ili kujenga
mazingira ya uhalisia, kongamano limetumia hali halisi ya nchi ya Somalia na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama mifano halisi inayotoa mafunzo kwa
ajili ya mjadala wa kongamano
|
|
Kamugisha alisema mwenyeji wa
kongamano hilo alikuwa Rais mstaafu Mkapa na waliohudhuria ni rais mstaafu wa
Afrika Kusini Thabo Mbeki na rais mstaafu wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na
washiriki wengine walitoka katika taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa
zinazojihusisha na masula ya usalama na kulinda amani.
|
Viongozi wastaafu Afrika waazimia mambo 5
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment