|
Serikali ya Tanzania imesaini
makubaliano ya msaada wa zaidi ya Shilingi Bilioni 146.4 na Serikali ya
Jamhuri wa watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu cha usafirishaji
pamoja na ujenzi wa reli ya kati ya kisasa ili kusaidia kusukuma maendeleo
Akizungumza baada ya kusaini
makubaliano hayo, Katibu Kkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bwana Doto James
amesema katika fedha hizo dola Bilioni 62 zimetolewa msaada kwa ajili ya
ujenzi wa chuo kikuu cha taifa cha usafirishaji huku kiasi kilichobaki
kitatumika kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kisasa
|
|
Balozi wa China hapa nchini Bi.
Wang Ke amesema serikali ya China imejipanga kuzisaidia nchi tano za Afrika
katika sekta ya usafirishaji kwenye maeneo matatu ikiwemo, Miundombinu,
usafirishaji pamoja na utaalamu ambapo kwa upande wa Tanzania tayari imeanza
na msaada wa ujenzi wa chuo kikuu cha usafirishaji pamoja na reli ya kisasa
|
|
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha
usafirishaji Profesa Zacharia Mganiliwa amesema ujenzi wa chuo kikuu hicho
utasaidia kupatikana wataalamu katika sekta mbalimbali watakaosaidia katika
miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo maboresho katika sekta ya usafirishaji
wa anga na reli, huku Kaimu Mkurugenzi wa reli Bwana Foxcusd Makoye
amepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya
usafirishaji.
|
Tanzania yapata msaada Bilioni 146.47
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment