Wadau waanza kuchukua hatua za kunusuru uhifadhi Manyara Tarangire

Serikali shirika la hifadhi za taifa na wadau wa uhifadhi wameanza kuchukua hatua  za kunusuru  Ikolojia ya hifadhi ya ziwa Manyara na Tarangire kwa kuimalisha maeneo ya mapito ya wanyamapori (SHOROBA) yanayoathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazotisha kukauka kwa ziwa Manyara na kutishia  kufunga mapito ya wanyamapori (SHOROBA) wanaokwenda na kurudi katika hifadhi za Manyara na Tarangire

Wakuu wa wilaya ya Karatu  Therecia Mahongo  anasema mpango huo unahusisha kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kilimo holela katika maeneo hayo na wanaoharibu mazingira kwenye mapito ya wanyamapori

Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara Noelia Myonga anasema shughuli za kibindamu zinazofanywa katika  maeneo ya miinuka  katika  wilaya za Karatu na Babati  kwa kiasi kikubwa zimeathiri ziwa Manyara  ambalo ndiyo tegemeo pekee la hifadhi hiyo.

Viongozi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi  pamoja na  maeneo ya mapito ya wanyamapori wanasema wameanza kushirikiana na uongozi wa hifadhi katika kukomesha tabia hizo.<br



Wadau waanza kuchukua hatua za kunusuru uhifadhi Manyara Tarangire Wadau waanza kuchukua hatua za kunusuru uhifadhi Manyara Tarangire Reviewed by KUSAGANEWS on May 24, 2018 Rating: 5

No comments: