Wataalamu wa sekta ya elimu
kutoka nchi za Afrika, Ulaya na Asia wameitaka Tanzania kuwekeza zaidi katika
kujenga uwezo wa mfumo wa elimu nchini ikiwemo uwezo wa walimu,maafisa elimu
pamoja na miundombinu ya elimu ili kukabiliana na changamoto ya ubora wa
elimu unaosababishwa na ongezeko kubwa la wanafunzi katika ngazi ya shule za
msingi na sekondari.
Wakizungumza katika kongamano la
kimataifa la kujadili ubora wa elimu nchini, baadhi ya wadau wamesema ujio wa
sera ya mpya ya mafunzo ya mwaka 2008 ambayo imetambua elimu ya awali kuwa
sehemu ya elimu ya msingi,pamoja na sera ya elimu bure imechangia kushuka kwa
ubora wa elimu baada ya wanafunzi wengi kuandikishwa kuliko idadi ya walimu
na kusababisha mwalimu mmoja kuwa na wanafunzi hadi 180
|
|
Awali akizungumza kuhusu malengo
ya serikali na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu, katibu mkuu wizara
ya elimu,sayansi na teknolojia Daktri Leonard Akwilapo amekiri moja ya
changamoto kubwa inayoikabili serikali kwa sasa ni ubora wa elimu baada ya
mipango ya kuongeza madarasa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
|
Ubora wa Elimu ya Tanzania wajadiliwa.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment