Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar
wamefanikwa kukamata Shehena ya Magaloni 740 ya mafuta ya Kula
ambayo yalikuwa yasafirishwe kwenda nje ya Zanzibar baada ya kubadilishwa
nembo ya awali na kuwekwa nembo ya Oki
Wakala wa Chakula na Dawa
Zanzibar-ZFDA-imefanikiwa kunasa shehena ya magaloni 740 ya mafuta ya
kula yaliyokuwa yasafirishwe nje ya Zanzibar baada ya kubadilshwa
nembo yake halisi na kuwekwa nembo ya Oki,magaloni hayo 740 yalikuwa
yamehifadhiwa ndani ya tawi la CCM makadara Zanzibar.
|
|
Akizumgumza na vyombo vya habari
katika eneo la operesheni hiyo makadara mjini Unguja ambapo magaloni hayo
yalikuwa yakigeuzwa nembo za asili ndani ya tawi hilo la CCM Makadara kaimu mkurugenzi mtendaji wa wakala huo Dkt. Khamis Ali Omar
amesema walipata taarifa na kuvamia eneo hilo wakati wa usiku na
kukuta shehena hiyo huku mmiliki huyo akitoweka na anatafutwa ,mtendaji
huyo amethibitisha kuwa mafuta ijayo yenye nembo ya Turkey yatoka Indonesia
|
|
Kuonekana kwa mafuta hayo ndani ya
tawi la CCM ilizua mjadala mkubwa na hofu ya tawi hilo kuhusika hata
hivyo akiongea kwa simu naibu katibu mkuu CCM Dkt. Abdulah Juma Mabodi
amekanusha CCM kuhusika kauli ambayo iliungwa mkono na katibu wa CCM
jimbo la Malindi Salum Juma Ali aliyefika kwenye tukio hilo,huku
mwakilishi wa kampuni hiyo ya Oki Zanzibar Salum Humud wa Sub
Sahara amesema ni mtindo ambao lazima upigwe vita na serikali.
|
|
Wakti zoezi la kutaka kuyaondosha
mafuta hayo likianza mmoja ya mtu anayetuhumiwa kuhusika na
zoezi hilo aliibuka na kudai yeye hajui chochote
n awalikuwawnatumiaeneo hulo kuhifadhi ndai ya tawi la ccm.
|
Mafuta ya Kula yakamatwa yakisafirishwa kupelekwa nje ya nchi Zanzibar
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment