Wadau wa sekta ya usarishaji
abiria kwa kushirikiana na chama cha Madereva wa Mabasi nchini
wamejipanga kusitisha huduma ya usafiri nchini nzima ili kushinikiza SUMATRA
kutekekeza agizo la Waziri Mkuu la kuwataka kukaa pamoja na wadau ili kufanya
mapitio ya sheria na kanuni hizo mpya kama njia kutafuta ufumbuzi wa
vipengele vinavyobishaniwa.
Wakizungumza katika stendi kuu ya
Mabasi Ubungo,mwenyekiti wa chama cha Madareva wa Mabasi Bwana Shabani Mdemu
ameitaka SUMATRA kusitisha kutoza faini kubwa zilizopo kwenye sheria na
kanunu mpya zinazobishaniwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu lililotaka
wakae pamoja kufanya mapitio ya shirikishi ya kanuni na sheria hizo mpya.
|
|
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
TABOA Bwana. Enea Mrutu amewataka madereva hao kusitisha mpango wa kutaka
kufanya mgomo kutokana na TABOA iko katika mchakato wa kuonana na viongozi wa
juu wa serikali ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizomo
katika sekta ya usafiri ikiwemo faini kubwa zinazotumika katika sheria na
kanuni mpya ambazo tayari waziri mkuu ameagiza zifanyiwe kazi kwa
kuwakutanisha wadau wote
|
|
Wakizungumza kitengo cha
mawasiliano cha wakala wa serikali wa uthibiti wa usafiri wa nchi kavu na
majini-SUMATRA- kuhusu malalamiko hayo, ambapo wamesema swala la utekelezaji
wa agizo la Waziri Mkuu liko katika ngazi za juu,ikiwemo ngazi ya wizara
uchukuzi.
|
|
Wadau wa usafirishaji watishia kugoma nchini.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment