Vitabu vyenye makosa vyawatia matatani watumishi 22


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema watumishi 22 wa Taasisi ya Elimu Tanzania wamesimamishwa kazi kwa kuisababishia Serikali hasara ya kuchapisha vitabu vyenye makosa

Ndalichako amesema Kuna watumishi 22 wa Taasisi ya Elimu wamesimamishwa kazi  na hawajaishia hapo bali wanangalia hatua za kuwachukulia sheria kwa kuisababishia Serikali hasara.

Profesa Ndalichako alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Felister Bura bungeni mjini Dodoma leo Mei 2, wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara ya elimu ya mwaka 2018/19.

Katika majibu yake, Profesa Ndalichako amesema ni kweli kuna makosa katika vitabu hasa baada ya wabunge kuliibua bungeni mwaka jana

“Hata vitabu mlivyosema ni vichache, tulivyopitia tulibaini vitabu 16 na tumevifanyia mabadiliko vya kuanzia darasa la kwanza, pili, tatu na nne na tumesimamia vyema kuchapwa upya,” amesema Profesa Ndalichako
Vitabu vyenye makosa vyawatia matatani watumishi 22 Vitabu vyenye makosa vyawatia matatani watumishi 22 Reviewed by KUSAGANEWS on May 02, 2018 Rating: 5

No comments: