Upelelezi kesi ya Mbunge Nasari ya 2014 umekamilika


Upelelezi kesi inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari kuhusu  kesi ya kumshambulia aliyekuwa Mtendaji wa kata ya Makiba, Neeman Ngudu ya mwaka 2014 umekamilika.

February 6 2018, Nassari alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa mashtaka ya kesi anayodaiwa kuifanya 2014 katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Jasmin Abdul ameahirisha kesi hadi June 6, 2018 ambapo mtuhumiwa atasomewa maelezo ya awali baada ya upande wa Jamhuri kusema upelelezi umekamilika.

Upelelezi kesi ya Mbunge Nasari ya 2014 umekamilika Upelelezi kesi ya Mbunge Nasari ya 2014 umekamilika Reviewed by KUSAGANEWS on May 02, 2018 Rating: 5

No comments: