SERIKALI YAHAMASISHA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

Serikali itaendelea kuhamasisha shughui za hifadhi ya Mazingira hususani kutunza vyanzo vya maji kwa kuendeleza kutoa miongozo ya utekelezaji wa sheria na mikakati inayohusisha kutunza vyanzo vya maji

Akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Catherine Magige, aliyeuliza serikali ina mikakati ipi kisheria kushughulikia suala la ulinzi wa maeneo ya vyanzo vya maji ili kunusuru maeneo hayo dhidiya uvamizi na matumizi mengine yasiyokusudiwa

Naibu waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Kangi Lugola amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuhamasisha jamii zinazozunguka vyanzo vya maji, serikali za mitaa na vijiji kushiriki katika jitihada za kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kuviwekea mipaka

Aidha Mheshimiwa Hasunga amesema uvamizi huo umesababisha baadhi ya maeneo ya hifadhi kupoteza sifa katika mapori tengefu 12 na hivyo kuanzisha mchakato wa kuyarudisha kwa wananchi ili yatumike kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji



SERIKALI YAHAMASISHA USIMAMIZI WA MAZINGIRA SERIKALI YAHAMASISHA USIMAMIZI WA MAZINGIRA Reviewed by KUSAGANEWS on May 02, 2018 Rating: 5

No comments: