|
Zaidi ya hekta 500 za mazao ya
Mahindi na Mpunga katika tarafa za Mng'eta na Mlimba wilayani Kilombero
zimeharibiwa vibaya na Panya walioibuka na kuvamia mazao hayo yaliyopandwa
shambani jambo lililosababisha hofu kubwa kwa wakulima kukosa mazao ya chakula
na biashara kwa msimu wa kilimo mwaka 2017-18 licha ya serikali kupambana
vikali kuwatokomeza Panya hao waharibifu
Akizungumza katika kikao cha
baraza la Madiwani katibu tawala wilaya ya Kilombero Robert Selasela kwa
niaba ya mkuu wa wilaya hiyo James Ihunyo amesema licha ya panya hao kuwa
tishio serikali imejitahidi ili kuona shuhuli za Kilimo zinaendelea
|
|
|
Kwaupande wake mwenyekiti wa
halmashauri hiyo bwana David Lugazio amesema pamoja na changamoto hiyo lakini
katika elimu halmashauri imejitahidi kuhakikisha elimu inasonga mbele na
kufanikiwa kupiga hatua kutoka nafasi 18 ya ufaulu hadi kufikia nafasi ya 11
jambo lilil pongezwa na katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Cliford Tandari na
kuwapa vyeti walimu waliofanya vizuri katika shule zao
|
PANYA WAHARIBU MAZAO KILOMBERO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment