Dk. Mpango akiri ongezeko la umaskini licha ya utajiri wa rasilimali


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema licha ya utajiri wa rasilimali uliopo nchini wananchi wameendelea kuwa maskini

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii Dar es salaam, Dk Mpango aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja sababu kubwa kuwa ni kutokuwepo kwa uwiano kati ya ukuaji wa uchumi na sekta ya Kilimo

Amesema Tanzania ni tajiri wa rasilimali ikiwemo maziwa kama Victoria, Tanganyika, Rukwa, Nyasa na mito mingi inayotoa fursa za uvuvi na uzalisha wa umeme pamoja utajiri wa madini kama dhahabu, almasi, Tanzanite, ruby, bati, chuma, mkaa, uranium, gesi ya asili, helium na mengineyo.

Ameongeza kuwa Tanzania ni kituo kikubwa cha utalii ikiwa na urefu wa kilometa 1,200 za fukwe za bahari, hifadhi za wanyama, huku  ikiwa nchi ya amani na utulivu isiyokuwa na machafuko ya kikabila

Hata hivyo,Dokta Mpango amesema uporaji wa maliasili umesababisha maisha ya Watanzania walio wengi kuwa masikini, huku wachache wakifaidi rasilimali hizo



Dk. Mpango akiri ongezeko la umaskini licha ya utajiri wa rasilimali Dk. Mpango akiri ongezeko la umaskini licha ya utajiri wa rasilimali Reviewed by KUSAGANEWS on May 02, 2018 Rating: 5

No comments: