Serikali
imesema hali ya ukame uliozikumba nchi za ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini
mwa Afrika mwaka 2017/18 umesababisha Tanzania kushindwa kufikia matarajio ya
sukari tani 314,000 na badala yake
imezalisha tani 300,399.
Akiwasilisha
bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ya mwaka 2018/19, waziri wa
wizara hiyo, Charles Mwijage amesema takwimu hizo ni za hadi kufikia Aprili 20,
2018.
Amesema
mahitaji ya sukari nchini ni takribani tani 630,000 kwa mwaka na kwamba kati ya
kiasi hicho tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 145,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
“Sukari kwa matumizi ya viwandani haizalishwi
hapa nchini. Uwezo wa uzalishaji wa ndani kwa sasa ni wastani wa tani 320,000
kwa mwaka. Pengo la mahitaji takriban tani 165,000 za sukari ya kawaida na tani
145,000 za viwandani huzibwa kwa kuagizwa kutoka nje ya nchi,”amesema.
Amesema
kampuni nne zinayozalisha sukari nchini ndizo zilizopewa jukumu la kuagiza
sukari kwa masharti kuwa hakutakuwa na upungufu wa sukari
nchini na ni lazima wapanue mashamba ya miwa ili ifikapo mwaka 2020 Tanzania ijitosheleze kwa sukari.
Amezitaja
kampuni zilizopewa jukumu la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuwa ni
Kilombero , TPC, Kagera na Mtibwa.
Ukame wakwamisha matarajio ya sukari nchini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment