Shirika
linalotetea haki za watu wanaotaka kufa limetangaza kuwa mwanasayansi David
Goodall, 104, aliyesafiri kutoka Australia hadi Uswizi ili kujitoa uhai
amefariki katika kliniki moja nchini Uswizi.
Mwanaikolojia huyo ambaye pia alikuwa mtaalamu
wa mimea hakuwa anaugua lakini alisema aliamua kujitoa uhai kutokana na
kudhoofika kwa 'ubora wa maisha yake'.
Goodall
alikuwa amezua mjadala kutokana na safari yake ya kutoka Australia kwenda
kujitoa uhai.
Muda mfupi
kabla ya kifo chake, alisema alikuwa na "furaha kuhitimisha" maisha
yake.
"Maisha
yangu yamekuwa dhaifu sana kwa mwaka mmoja hivi uliopita na hivyo basi nina
furaha kuyahitimisha," alisema akiwa amezingirwa na jamaa wake kadha.
"Nafikiria,
kuangaziwa kwa kisa changu kutachangia kutetea haki za wazee kuruhusiwa kujitoa
uhai, jambo ambalo nimekuwa nikitaka."
Alifariki leo
saa sita na nusu mchana katika kliniki ya Life Cycle mjini Basel baada ya
kudungwa sindano ya Nembutal, kwa mujibu wa Philip Nitschke mwanzilishi wa
shirika la Exit International lililomsaidia kujitoa uhai.
"Najuta
kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya
kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia.
Aliyedaiwa
kufariki azinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti
"Sina
raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu
anazuiwa kufa."
Ni jimbo
moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala
mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua
mahututi.
Madaktari wamsaidia mzee wa miaka 104 kujiua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment