Wizara ya
mambo ya ndani nchini imesema mbunge wa
Mbeya Mjini Joseph Osmund Mbilinyi,(Sugu) aliyefungwa jela baada ya kupatikana
na kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli aliachiliwa
huru kwa msamaha wa Rais.
Kamishna
Jenerali wa Idara ya Magereza Juma Malewa amesema hakufai kuwa na utata kuhusu
kuachiliwa huru kwa mbunge huyo.
Bw Mbilinyi,
maarufu kama Sugu, alifungwa katika gereza la Ruanda, Mbeya mnamo 26 Februari
baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano na mahakama ya hakimu mkazi Mbeya.
"Mfungwa
huyo kama wafungwa wengine mara baada ya kupokelewa gerezani alipata msamaha wa
theluthi moja ya kifungo chake na hivyo alitakiwa kuachiliwa huru tarehe 5 Juni
2018," amesema Dkt Malewa.
Mbunge
afungwa jela miezi mitano kwa kumtusi Magufuli Tanzania
Majaliwa
awaonya walioweka mafuta na sukari kwenye mabohari
Rais
Magufuli mnamo 26 Aprili wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano alitoa
msamaha wa robo moja kwa adhabu ya wafungwa waliokuwa na sifa za kunufaika na
msamaha wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 45(1)d ya Katiba ya Tanzania.
Masharti ya
msamaha huo ni kwamba lazima mfungwa awe ametumikia robo moja ya adhabu yake
baada ya kuondolewa theluthi moja ya kifungo.
Idara ya
magereza imesema chini ya utaratibu huo kuna wafungwa 3,319 waliofaidika na 585
kati yao waliachiliwa siku hiyo ya Sikukuu ya Muungano.
"Walibakia
gerezani kumalizia sehemu ya vifungo vyao na kuendelea kuachiliwa kadiri ya
tarehe zao ambapo mfungwa aliyekuwa namba 219/2018 Joseph Osmund Mbilinyi
maarufu Sugu ni miongoni mwa wafungwa walionufaika, na msamaha wa rais na
ameachiliwa leo tarehe 10 Mei, 2018 badala ya 5 Juni 2018 kwa mujibu wa
sheria," amesema Dkt Malewa.
"Hivyo
basi mfungwa namba 219/2018 Joseph Osmund Mbilinyi alipata msamaha huo kutokana
na mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Katiba."
Sugu, ambaye
ni mbunge kwa tiketi ya chama cha upinzani Chadema, aliachiliwa huru pamoja na
mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga,
ambaye walifungwa pamoja baada ya kupatikana na makosa sawa.
Walidaiwa
kutenda kosa hilo katika mkutano wa hadhara walioufanya 30 Desemba mwaka jana
eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Akizungumza
baada ya kuachiwa huru, mbunge huyo ameishutumu serikali na kusema kwamba
alifunhwa "kiholela", kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.
"Sikutaka
kuhoji sababu za kutolewa, jana niliambiwa jiandae kesho (leo) tutatoka, basi nasi
tukasema haina shida kwa sababu sikuwa na sababu ya kuwa ndani. Naamini
sikutakiwa kuwa gerezani."
Kishindo cha Sugu mtaani baada ya kuachiliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 10, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment