Uchunguzi waliosafirisha korosho na kuzichanganya na mawe wakamilika


Serikali imetangaza kukamilisha uchunguzi  uliolenga kuwabaini waliosafirisha korosho nje ya nchi na kuzichanganya na mawe

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 25, 2018 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa

Amesema wakikamilisha uchunguzi wa kina, Serikali itapeleka taarifa bungeni

Amesema tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kuhakikisha jambo hilo halijirudii,  baadhi ya waliohusika wameanza kuchukuliwa hatua

Alieleza hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasai (CCM) aliyehoji  hatua zilizochukuliwa na Serikali kwa walioruhusu korosho  zilizochanganywa na mawe kusafirishwa nje ya nchi bila kuchaguliwa

Amesema ilibainika baada ya makontena mawili ya korosho ghafi kutoka Tanzania kugundulika kuwa zimechanganywa na mawe pamoja na korosho nzuri na mbaya kwa lengo la kuharibu soko la dunia

Kuhusu soko la korosho ghafi, Dk Mwanjelwa amesema lilikuwa zuri katika msimu wa 2017/18 korosho ziliuzwa kuanzia Sh3,500 hadi Sh 4,000 kwa kilo

Uchunguzi waliosafirisha korosho na kuzichanganya na mawe wakamilika Uchunguzi waliosafirisha korosho na kuzichanganya na mawe wakamilika Reviewed by KUSAGANEWS on May 25, 2018 Rating: 5

No comments: