Spika Ndugai aketi sehemu ya wageni, atambulishwa kama mgeni


Imezoeleka kumuona Spika Job Ndugai akiongoza kikao cha Bunge au kuketi ndani ya ukumbi wa Bunge kama ilivyo kwa wabunge wengine.

 Lakini leo Ijumaa Mei 25, 2018 hali ilikuwa tofauti baada ya kuketi eneo maalumu kwa ajili ya wageni ndani ya ukumbi huo akiwa sambamba na mgeni wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma

Wakati Ndugai akiwa katika eneo hilo, kikao cha Bunge kilikuwa kikiongozwa na mwenyekiti, Mussa Azzan Zungu ambaye alionyesha kushangazwa na kitendo hicho akidai ni jambo lisilo la kawaida

“Hii itaingia katika historia ya kitabu cha  Guiness Book (kitabu cha maajabu duniani). Hili  ni la pekee nikiamini kuwa hata wapiga picha mtakuwa mmepata picha nzuri sana, asante Spika,” amesema Zungu

Baada ya utambulisho huo, Ndugai na mgeni wake walisimama na kushangiliwa kwa nguvu na wabunge kabla ya kuondoka wakipitia mlango wa  wageni wa kawaida kisha wakazunguka kwenda ofisi ndogo ya Spika iliyopo nyuma ya ukumbi wa Bunge.
Spika Ndugai aketi sehemu ya wageni, atambulishwa kama mgeni Spika Ndugai aketi sehemu ya wageni, atambulishwa kama mgeni Reviewed by KUSAGANEWS on May 25, 2018 Rating: 5

No comments: