TMA yatoa tahadhari mvua kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani kwa siku tano mfululizo zinazoweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TMA, mvua hizo zimeanza jana Mei Mosi na zitaendelea mpaka Mei tano mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja

Mikoa mingine itakayoathirika na mvua hizo ni Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara

TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni pamoja na mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuathiri jamii, adha ya usafiri kwa barabara kubwa kutopitika

Kwa mujibu wa TMA athari za mvua hizo ni kujaa kwa maji au yanayopita kwa kasi na kuhamishwa kwa watu kutoka maeneo yaliyoathiriwa

Angalizo lingine ni upepo mkali na mawimbi makubwa kwa maeneo ya ukanda wa Pwani inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja 
TMA yatoa tahadhari mvua kubwa TMA yatoa tahadhari mvua kubwa Reviewed by KUSAGANEWS on May 02, 2018 Rating: 5

No comments: